Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amesema kuwa alishukuru sana kwa kitendo cha Mwana FA kumpa ushirikiano kwenye kazi zake na kupost Instagram kumpa promo ya wimbo wake mpya.

Lady Jaydee amesema ni jambo jema na la kumshukuru Mungu kwa wasanii wanapopeana ushirikiano.

“Ni jambo jema msanii mwenzako anapokusuport, na ndio kitu ambacho wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu kwa hivyo mkae mkifahamu kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisuport”,.

Lady Jaydee ameendelea kwa kusema kuwa “ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri, watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.

Wawili hao walikuwa kwenye bifu kali ambalo ilikuwa hata salamu hakuna, lakini hivi karibuni wameamua kuyamaliza na kuondoa tofauti zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *