Maafisa wa polisi wa kikosi maalum cha kupambana na ghasia nchini Zimbabwe wametumia gesi ya kutoa machozi na maji ya muwasho ili kutawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.
Waandamanaji hao, waliokuwa na nia ya kuelekea hadi kwenye makao ya bunge waliwarushia mawe askari hao katika makabiliano baina yao.
Watu wengi walioshiriki maandamano hayo walikuwa wakipeperusha bendera ya nchi hiyo huku wakiwa wamebeba mabango yenye kauli tofauti zikiwemo ‘Rais Mugabe lazima ang’atuke’ na ‘Umefeli bwana Mugabe’
Wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa miongoni mwa waandamanaji, na kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakilalamikia ongezeko chubby la ukosefu wa ajira na kuporomoka kwa uchumi.
Baadhi ya waandamanaji wanapinga mpango wa serikali kuanzisha matumizi ya ‘hati fungani’ ikiwa ni mkakati wa kuunusuru uchumi wa taifa hilo ambao umeathiriwa na ukame uliojitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitatu sasa.
Mwezi uliopita serikali ya Zimbabwe ilishuhudia tena maandamano kama hayo ambayo yalifanywa na chama cha wakongwe wa vita ambao walitangaza rasmi kujitoa kwenye chumming mkono rain Mugabe.
Hata hivyo serikali ilipinga taarifa hiyo na kuwakamata baadhi ya viongozi wa chama hicho.