Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Katika mabadilko hayo Rais Magufuli ameongeza wizara mbili hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo hapo awali.

Rais Magufuli amezigawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake, pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili tofauti.

Sambaba na hilo pia Rais Magufuli amemteua Mh. George Haruna Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9 mwaka huu Ikulu jijini Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *