Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala amesema serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe kwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Waziri Kigwangala ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagrama, ambapo ameeleza kwamba watendaji hao wanachelewesha maendeleo ya nchi, hivyo watafikisha taarifa kwa mwenye mamlaka zaidi ili wachukuliwe hatua.

Ameanza kwa kuandika “Halmashauri chache zenye viongozi na watendaji wazembe zitabaki nyuma. zitatuangusha. Hatuko tayari kuvumilia, tutapendekeza kwa mwenye mamlaka hatua kali zichukuliwe”,.

Dkt. Kigwangala ameendelea kwa kuandika kwamba kutokana na watu hao wanaingiwa na mashaka kuwaacha wasimamie miradi mikubwa ambayo inapaswa kutekelezwa, ikiwemo uboreshaji wa vituo vya afya, kitendo ambacho kinawatesa wananchi.

Pia ameandika “Wizara ya Afya tumepata wafadhili ambao watatuwezesha kuboresha vituo vya Afya150 kwa kupeleka milioni za kitanzania 500 kwenye kila Kituo. Pesa hizi bado hazijaenda kwenye halmashauri mpaka sasa. Nachelea kusema tukiwapelekea viongozi na watendaji wa namna hii wanaweza kushindwa kuzisimamia ipasavyo, kuacha kupeleka ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia”,.

Hivi karibuni waziri Kigwangala amekuwa akifanya ziara kwenye vito vya afya mbali mbali nchini, kutathmini changamoto ambazo zinavikabili na kuvitafutia njia za ufumbuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *