Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Rais Magufuli hakuwahi kuwa na nafasi ya uongozi ndani ya Chama hicho.
Polepole amesema kuwa Rais Magufuli ndiye alikuwa mtu sahihi 2015 kwani alipoingia ndani ya chama na serikali ameweza kuona matatizo ambayo wengine hawakuweza kuyaona.
Amesema kuwa kwa jinsi ambavyo chama hicho kilivyokuwa kipindi cha nyuma kilihitaji mtu ambaye hayupo ndani ya mfumo wake ili aweze kuona mapungufu mbalimbali ndani ya chama na serikali.
Aidha Polepole amesema kuwa Rais Magufuli alipoingia serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi hakuona haya kusema madudu na uozo uliopo ndani yake
Pia amesema kuwa anapomsikia Rais Magufuli akisema kuwa nafasi ya Urais ni kazi ngumu anamuelewa kweli na kusema kuwa yeye anajua uongozi si kazi ya furaha bali ni mzigo mkubwa.