Nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta leo amesaini mkataba mpya wa maisha na klabu yake hiyo.

Mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa  miaka 33 ameichezea Barcelona mara 639 ikiwa na wa pili kushiriki mechi nyingi na timu hiyo na kufunga mabao 55.

Iniesta alikuzwa na shule ya magfunzo ya soka ya Barcelona kwa jina La Masia baada ya kujiunga akiwa na umri wa miaka 12.

Alishiriki mechi yake ya kwanza mnamo mwezi Oktoba 2002 na amefanikiwa kushinda mataji 8 ya ligi ya Uhispania na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya.

Iniesta anekuwa nahodha wa timu hiyo tangu 2015 na anagawana rekodi ya kushinda mataji mengi na Lionel Messi kwa kushinda mataji 30 katika historia ya Berclona.

Ameshinda kombe la Yuro mara mbili na Uhispania na kuweza kufunga bao la dakika za lala salama katika kombe la dunia la 2010 dhidi ya Uholanzi nchini Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *