Aliyekuwa kocha wa Everton, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji akichukua nafasi ya Marc Wolmosts aliyejiuzuru baada ya kufungwa na kutolewa na Wales katika michuano ya Euro nchini Ufaransa.
Martinez mwenye miaka 43 pia aliwahi kuzifundisha timu za Wigan na Swansea alifukuzwa kazi na Everton mwezi Mei mwaka huu baada ya kufanya vibaya katika mashindani mbali mbali akiwa na timu hiyo.
Kocha huyo raia wa Uispania alidumu miaka mitatu Goodison Park baada ya kurithi nafasi ya David Moyes.
Taarifa ya kazi ya ukocha wa kuifundisha timu hiyo ilitangazwa wazi mtandaoni na Shirikisho la Soka nchini Ubelgiji.
Shirikisho hilo lilisema linamtafuta mtu bingwa katika mawasiliano na mwenye uwazi na ambaye amethibitisha uzoefu katika kuwapa wachezaji nyota ujuzi na ustadi katika ufundi.
Marc Wilmts: Kocha aliyejiuzuru Ubeligiji.