Aliyekuwa kiongozi wa wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria Abubakar Shekau amepinga tangazo la kundi la Islamic State kwamba kundi hilo limepata kiongozi mpya.
Kundi la IS hapo jana limetangaza kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa wapiganaji hao nchini Nigeria.
Lakini Abubakar Shekau, ambaye hajaoneakana kwa kipindi cha mwaka mmoja, amemweleza kiongozi huyo mpya kama mtu mwenye kuamini miungu wengi na ambaye ameenda kinyume na mafunzo asili ya Boko Haram.
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya usalama anasema bado ni mapema mno kujua iwapo Nigeria na nchi nyingine za Afrika Magharibi zinaweza kutumia mgawanyiko huo katika kundi hilo kukabiliana nalo.