Watu 15 wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari la mizigo aina ya Fuso lililokuwa likitokea Sumbawanga mjini na kwenda Wampembe mwambao mwa ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Lori hilo aina ya Fuso mali ya Bwana Bakari Kessy likiwa limebeba shehena ya viroba vya mahindi na watu 28 ndani yake lilipinduka baada ya dereva kukata kona akiwa kwenye mwendokasi kisha gari kumshinda dereva na kusababisha vifo vya watu 15 ambao walikuwa wamepanda kwenye gari hilo la mizigo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Geoge Kyando, gari hilo lilikuwa likitoka Sumbawanga kuelekea Wampembe katika mwambao wa ziwa Tanganyika.
Polisi wamedai gari hilo ni mali ya mtoto wa mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy Mohamed anayefahamika kwa jina la Bwana Bakari Kessy.