Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.

Ameshtakiwa pamoja na mama yake mzazi aitwae Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.

Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda ambapo rais Kagame alishinda kwa kishindo.

Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.

Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.

Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono ugombeaji wake.

Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi nchini humo pamona na ndugu zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *