Wananchi wa jimbo la Catalonia leo wanatarajia kufanya mgomo kufuatia kura ya maoni yenye utata nchini Uhispania.
Mgomo huo ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi huko Catalonia, unalalamikia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa wakati wa kura ya maoni ya siku ya Jumapili.
Uhispania imeitaja kura hiyo ya maoni kuwa iliyo kinyume na sheria. Hata hivyo zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga kura.
Lakini mimia ya watu walijeruhiwa wakati polisi wa Uhispania walijaribu kuzuia zoezi hilo kuendelea.
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Catalonia yajiandaa kufanya mgomo kulalamikia ghasia za Jumapili
Baadhi ya maafisa walioamrishwa kuwazuia watu wasipige kura walionekana wakifyatua risasi za mipira, wakivamia vituo vya kupigia kura na kuwavuta wanawake kwa nywele zao.
Mgomo huo wa leo Jumanne utavuruga shushuli za usafiri wa umma, shule na zahahati huko Catalonia.
Klabu maarufu cha kandanda cha Barcelona pia inatarajiwa kugoma, licha ya kuwa hawachezi mechi huku vyuo vya umma na makavazi nayo yakitarajiwa kugoma.