Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amefunguka na kusema kuwa ndoa yake na mpenzi inaweza kufanyika mwakani lakini kwa sasa bado kidogo mipango  ya harusi haijafanyika.

Msanii huyo ambae miezi kadhaa hivi iliyopita alichumbiwa na mchumba wake mwenye asili ya kizungu anasema kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwakani.

Amesema kuwa ana uhakika michongo yote ya harusi itaenda vizuri lakini kwa utaratibu wake na kazi zake kwa sasa  hana mpango wa kufunga ndoa  mwaka huu hadi mwakani.

Maua ameendelea kusema kuwa anamshukuru sana Mungu maana ameweza kumsimamia na kuweka kukaa kwenye game muda mrefu huku nyimbo zake zikifanya vizuri ,lakini pia ameelezea sababu za msanii kukaa katika game la muziki  kwa muda mrefu ni vile ambavyo msanii anaamua kujiweka.

Maua Sama amekuwa mmoja wa wanadada wanaofanya vizuri kuanzia katika wimbo wake wa ‘Mahaba niue’ ambao ulikaa muda mrefu kwenye chati, lakini hata baada ya wimbo huo nyimbo zilizofuata ziliendela kufanya vizuri na kupokelewa vizuri na mashabiki wake, akiwa pia ni mmoja wa wasanii wanaozunguka mikoani katika tamsha la Fiesta , maua amekuwa akipokelewa vizuri katika jukwaa la Fiesta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *