Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amekanusha taarifa kuwa yeye ndiyo chanzo cha Baraka The Prince kutoka lebo ya RockStar4000.
Ommy Dimpoz amesema kuwa siyo kweli kama Baraka The Prince ametoka kwenye lebo hiyo baada ya yeye kujiunga na lebo hiyo nchini ambayo ina mmiliki mwanamuziki Alikiba.
Baraka The Prince alikuwa ndani ya lebo hiyo lakini alihama na siku chache lebo hiyo ikamsainisha mwanamuziki Ommy Dimpoz akiwa mwanamuziki mpya ndani ya lebo hiyo maarufu nchini.
Ommy ambaye kwsasa anatamba na wimbo wake ‘Cheche’ amesisitiza kuwa sababu za Baraka kuhama ndani ya lebo hiyo yeye azijui kwasababu wakati anasaini na lebo hiyo Baraka alikuwa tayari ameshaondoka.
Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa si kweli kwamba yeye kuingia RockStar4000 ndiyo sababu ya Baraka The Prince kutoka kwenye menejimenti hiyo iliyochini ya Seven Mosha.
Pia Ommy ameeleza kuwa kwanza hawana bifu, na walifahamiana miaka mingi hivyo hawezi kujua kilichomuondoa Baraka kwenye lebo ya RockStar4000.
Kuhusu RockStar4000 kupata pengo baada ya Baraka kuondoka, Ommy amesema kuwa hawezi kulisemea hilo au kujua kwa sababu wakati Baraka yupo RockStar4000 yeye hakuwepo kwa hiyo hajui chochote kuhusu Baraka The Prince kuondoka kwenye lebo hiyo.