Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Mh. Temba amefunguka kwa mara ya kwanza sababu iliyofanya kundi la Yamoto Band kuvunjika.
Temba ambaye kwasasa anaisimamia kituo cha Mkubwa na Wanawe ameamua kuweka suala la kuvunjika kwa kundi hilo baada ya kukutana na maswali kila wakati.
Temba amesema majungu yaliyopikwa na watu wa nje na tamaa za kuwa na wasanii hao ambao wao wamehangaika kuwatoa kuanzia chini, ndio sababu kubwa ya kundi hilo kusambaratika.
Msanii huyo amesema kuwa kuna watu walikuwa wakitamani kuwasimamia wasanii hao mmoja mmoja na sio kundi zima.
Kundi hilo kwasasa limevunjika na kila mmoja anafanya kazi peke yake kama solo artist baada ya kusambaraika ambapo baadhi yao wameshaachia nyimbo.