Nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, LeBron James amewapongeza wachezaji wa ligi ya soka ya Marekani NFL ambao wamefanya mgomo dhidi ya rais Donald Trump.

Jamese amesema amemtuhumu rais huyo wa Marekani kwa kutumia michezo ili kujaribu kugawanya watu.

Trump alinukuliwa akisema siku ya Ijumaa kwamba wachezaji wa ligi ya NFL ambao walishindwa kusimama wakati wa wimbo wa taifa walifaa kufutwa kazi ama kusimamishwa kwa mda.

Katika maandamano makubwa wikendi iliopita , wachezaji walijibu kwa kupiga goti moja chini huku wengine wakiamua kusalia katika chumba cha maandilizi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema kuwa hatomruhusu mtu mmoja licha ya uwezo wake kutumia michezo kama kigezo cha kutugawanya.

James ambaye anaichezea Cleveland Cavaliers na amewahi kushinda mataji matatu ya NBA alimfanyia kampeni Hillary Clinton, ambaye alikuwa mpinzani wa Trump wakati wa kinyang’anyiro cha urais cha mwaka 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *