Mkuu wa Wilaya ya Handeni,  Godwin Godwe amekabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha Kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.

Akizungumza wakati akikabidhi ardhi hiyo katika kijiji cha Kitumbi, Handeni mkoani Tanga, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo na maendeleo katika kijiji hicho ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli kuendeleza nchi ya viwanda na biashara.

Wadau wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza wakiwemo wasanii wa filamu, muziki na wachezaji mpira wa zamani wameamua kushiriki katika maendeleo ya taifa kwa kujihusisha na kilimo tofauti na kazi zao za kila siku za sanaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, msanii Steve Nyerere alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Gondwe na vingozi wa kijiji kwa kuwapa eneo la kuwekeza katika sekta ya kilimo.

Amesema kuwa “Sisi tunawashukuru wote kwa moyo mliotuonyesha, hatuna cha kuwalipa bali tutapambana kwa nguvu zetu ili kutimiza malengo ya eneo mlilotupa, Uzalendo Kwanza.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid amewakaribisha wasanii hao kwa mikono miwili na kuwaomba wawasaidie kumalizia ujenzi wa zahanati yao ambao umekuwa ukisua sua kutokana na kukosekana kwa fedha.

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *