Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema kuwa hakupendezwa na kauli ya Young Dee kumuita kifaranga.
Kauli hiyo ya Dogo Janja imekuja kufuatia siku za hivi karibuni Young Dee kusema kuwa hawezi kufananishwa na Dogo Janja pamoja na Young Killer kwani hao ni vifaranga vyake kwenye muziki.
Kutokana na kauli hiyo ya Young Dee, Dogo Janja amesema kuwa hakupendezwa na msanii huyo mwenzake kumuita kifaranga wake wakati kwenye muziki wote wmeanza kitambo.
Dogo Janja amesema kuwa “Mimi pia sipendi kufananishwa na kifaranga japo sijakataa kufananishwa na Young Killer kwa sababu alishawahi kuwa role model wangu, kwa hiyo kufananishwa naye si kitu kibaya, lakini kufananishwa na mla unga Young Dee ndiyo sipendi tena mnakosea kabisa.
Pia ameongeza kwa kusema “Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani tuzungumze lakini kufananishwa naye sasa hivi sitaki kwani ni mtu ambaye ukimuacha nyumbani kwako unawaza vitu vyako kama TV, radio na vingine. Je, utavikuta salama, maana asije kuiba kwenda kuuza,”.