Ni mara ngapi kwenye maisha umeona watu wenye utajiri, mali, fedha na dhamana kubwa ya madaraka wameweza kuishi maisha yanayofanana na watu wasio katika hadhi zao?
Ni viongozi wachache duniani wenye haiba hii, wenye utamaduni wa kutoyumbishwa na mali walizonazo au dhamana ya mamlaka waliyonayo.
Kila mmoja katika hawa ana sababu zake za kuwa hivi ingawa jambo linalowaunganisha pamoja watu hawa ni ukweli kuwa hawa ni MASTAA.
Sifa kubwa sana ya STAA wa kweli ni kutowaacha nyuma mashabiki wao au watu wanaowaongoza.
Mmoja wa watu wenye haiba hiyo ni mfalme wa nchi ya Dubai iliyopo kwenye falme za kiarabu, Sheikh Mohammad Bin Rashid Al Maktoum ambaye pia ni makamu wa rais na waziri mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mtawala huyu ameendelea kuongoza kwa kuwavutia watu wa hali ya chini kwa kupenda kujumuika nao na kushiriki kwenye mambo ya kijamii hususani yanayohusu watu hao.
Hebu tazama ustaa huu kisha kama nawe ni staa au ungependa kuwa staa tungependa kupata picha na video zako ukishiriki mambo ya kijamii ili tukutangaze na mashabiki wako aweze kuhamasika.
* Wasiliana nasi kwa kujaza fomu hapo chini.
MASTAA HAO NI KAMA IFUATAVYO