Rais wa kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais ni mapinduzi ya mahakama nchini humo.

Viongozi hao wawili walikuwa wakijibu uamuzi kamili wa mahakama ambapo majaji wa mahakama ya juu walitoa sababu zao kwa nini walifutilia mbali matokeo hayo ya urais.

Idadi kubwa ya majaji hao walisema kuwa matokeo hayo hayakuwa na ‘uwazi wala kuhakikiwa’.

Viongozi hao wawili hatahivyo waliangazia uamuzi wa majaji wawili waliopinga uamuzi hao ambao walisema kuwa kesi iliowasilishwa katika mahakama hiyo haikuwa na uzito wowote.

Rais Kenyatta alisema kuwa hakuna uchaguzi uosikumbwa na makosa madogo madogo kama ilivyotokea kwenye uchaguzi wa nchi hiyo.

Amesema kuwa mafanikio yote ya katiba mpya ilioidhinishwa 2010 yamepotezwa na uamuzi huo ambao umewawacha watu wachachee kuongoza dhidi ya walio wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *