Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa wao wanatoa taarifa ya maendeleo ya Tundu Lissu kulingana na madaktari wanavyowaambia.

Freeman Mbowe amesema kuwa wao hawawezi kusema chochote nje ya wataalam hao ambao ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua hali ya mgonjwa kwa kuwa ndiyo watu ambao wanakaa naye muda mrefu na kutambua maendeleo yake.

Aidha kiongozi huyo amezidi kuwaomba Watanzania kuzidi kumuombea Tundu Lissu na kuendelea kuchangia gharama za matibabu kwa kiongozi huyo kwani gharama za matibabu yake ni kubwa.

Mbowe amesema kuwa kutokana na gharama kuwa kubwa wao kama chama peke yao hawawezi kumudu hivyo ameomba Watanzania kuendelea kuchangia ili kiongozi huyo aendelee kupata matibabu na aweze kupana na kurejea nchini akiwa salama.

Tundu Lissu yupo mjini Nairobi Kenya kwenye matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa na kwenda Kenya kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *