Serikali kupitia mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo imelifungia gazeti la kila wiki la MwanaHalisi kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kuandika habari zinazokiuka taaluma ya habari.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na msemaji wa serikali, Hassan Abas amesema kuwa serikali imeamua kulifungia gazeti hilo baada ya jana kuchapisha habari yenye kichwa cha habari iliyosema ‘Tumuombee Magufuli au Tundu Lissu’.
Abas amesema kuwa wamefikia hatua ya kulifungia gazeti hilo baada ya kukaidi maelekezo ya kujirekebisha na habari zao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa gazeti hilo limekuwa likiandika kitu kinachafanana na habari na si uandishi wa habari.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewataka waandishi wa habari kuandika taarifa zenye ukweli ili kukuza taaluma hiyo.