Umoja wa Mataifa  (UN) umetahadharisha kuwepo kwa hali mbaya ya kibinaadam nchini Sudan kusini kutokana na mapigano kuanza tena upya na maelfu ya watu wakiyakimbia makazi yao kutokana na machafuko.

Shirika la kuhudumia wakimbizi linasema njaa na maradhi vinatishia maisha ya maelfu ya watu ambao wamebaki nchini humo.

Makundi ya watu wenye silaha pia yamewazuia watu wengi kuingia nchi jirani ya Uganda na kuna ripoti ya kuwepo na vitendo vya watoto kusajiliwa kwa nguvu kwenye jeshi.

Upungufu mkubwa wa chakula na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu umefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Mpango wa kumaliza mapigano kati ya Serikali ya Rais Salva Kiir na mpinzani wake mkubwa Riek Machar ulivunjika mwezi uliopita.

Katibu mkuu wa masuala ya kibinaadam wa umoja wa Mataifa, Stephen Obrien amesema mahitaji ya Sudani kusini ni Changamoto kubwa  watu wengi wanahitaji huduma, wanahitaji kusaidiwa, lakini zaidi wahitaji kulindwa.

Hivyo tunahitaji si tu kutazama maeneo yanayozunguka kambi hapa, lakini tunapaswa kutazama nje pia na kufikiria namna gani wau hawa watalindwa dhidi ya machafuko.

Kwenye machafuko hayo wanaoathirika ni watoto na wanawake, wagonjwa na walemavu wanaohitaji msaada nchini humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *