Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskeli za kisasa 200 kwaajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam.
Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwa kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana.
Kwa upande wa Kamanda Mambosasa amemshukuru Makonda kwa msaada huo kwani utalisadia jeshi la Polisi kuimarisha kazi zake za kulinda raia na mali zao ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Kupatikana kwa vitendeakazi hivyo ni matokeo ya jitiada binafsi za Makonda kutafuta Wahisani kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa kwa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam.
Makonda amesema kuwa sababu ya kutafuta kwa wahisani hao ni kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo magari, pikipiki za kawaida na za Traffic, Baiskeli za doria, silaha na Computer ili kuwarhisishia mazingira mazuri ya kufanyia kazi.