Tajiri mmoja raia wa China anayeishia mjini New York ambaye amewalaumu maafisa wa vyeo vya juu nchini China kwa kuhusika kwenye ufisadi ameomba kupewa hifadhi nchini Marekani.

Guo Wengui ambaye pia anafahamika kama Miles Kwok, anaamini kuwa anaonekana kuwa mpinzani wa utawala wa China.

Vyombo vya habari vimamemlaumu tajiri huyo wa umri wa miaka 50 kwa kumpa hongo naibu waziri mmoja, madai ambayo bwana Guo anayakataa.

Bwana Guo ambaye aliondoka China mwaka 2014, amechapisha ujumbe kadha katika mitandao ya twitter na YouTube zinazofichua ufisadi baina ya wanachama wakuu wa chama cha kikomisti cha China.

Pia ametoa kile kinachodaiwa kuwa siri za serikali kabla ya mkutano mu wa chama cha kikominist unaofanyika baada ya kila miaka mitano na ambao unatarajiwa kuanza Oktoba mwaka 18.

Mwezi Aprili serikali ya China ilitoa agazi kwa polisi wa kimqtaifa wa Interpol kutaka Bw. Guo akamatwe.

Mamlaka za China pia zinaripotiwa kumchunguza Bw. Gao kwa takriban uhalifu 19 ukiwemo utekaji nyara na ulanguzi wa pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *