Chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta kimewakataa maofisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya wa Urais mwezi ujao Oktoba 17.

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maofisa hao, ambao kimesema wanawafahamu kuwa wanapendelea wapinzani.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza maofisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba 17 ambapo miongoni mwa maofisa hao ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na msimamizi wa kituo cha Taifa cha kujumlishia matokeo.

Rais Uhuru amekutana na viongozi wa kidini ikulu ambapo amesema tarehe iliyotangazwa inafaa ili kutovuruga kalenda ya mitihani ya taifa ambayo imepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Mahakama ya Juu nchini Kenya ilifuta matokeo ya Urais  kwa kudai ulikuwa na dosari ambapo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 ambao Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *