Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea wakati viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.
Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya kupitia taarifa yake imesema kuwa viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja la Uredi.
Idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.