Kiungo wa Tottenham, Dele Alli uhenda akakumbwa na rungu la FIFA baada ya kuonyesha kidole cha kati wakati wa mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Uingereza na Slovakia.

Kitendo hiko kinahisiwa kuwa alikua amekusudia kumtusi mwamuzi, kutokana na kukerwa na maamuzi yake kwenye mchezo huo.

Kitendo hicho hakikuonwa na mwamuzi Clement Turpin kutoka nchini Ufaransa, na kimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari, kutokana na picha zilizopigwa na waandishi wa habari waliokua wanafuatilia mpambano huo uliomalizika kwa England kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Hata hivyo Dele amesema hakua na kusudio ovu kama inavyochukuliwa na kuelezwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, bali alifanya hivyo ikiwa ni ishara ya kumtania aliyekua mchezaji mwenzake wa Spurs Kyle Walker ambaye kwa sasa anaitumikia Man city.

Dele  mwenye umri wa miaka 21, tayari ameshawaomba radhi wadau wa soka waliokipokea kwa hisia mbaya kitendo hicho, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, na ameendelea kusisitiza hakua na nia mbaya.

Shirikkisho la soka duniani FIFA, linatarajiwa kufuatilia kwa kina kitendo hicho kupitia kamati yake ya nidhamu, na kama watabaini kiungo huyo alikusudia kumtusi mwamuzi Turpin, huenda wakamfungia michezo minne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *