Kampuni ya inayojishughulisha na uchimbaji madini ya Acacia imesema kuwa itapunguza wafanyakazi na shughuli zake za migodini ikiwa ni sehemu ya athari ya uzuiaji wa usafirishwaji wa makinikia uliowekwa na serikali ya Tanzania mwezi Machi mwaka huu.
Kampuni hiyo imesema kuwa baadhi ya shughuli ndani ya mashimo yake ya dhahabu zitasimama, ndani ya wiki nne, uchenjuaji wa makinikia pia nao utasimama.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa la London nchini Uingereza imesema kuwa kusimamishwa kwa usafirishwaji wa makinikia kumekuwa kukiikosesha takribani $15 milioni (Dola milioni kumi na tano) kwa mwezi.
Hata hivyo, Acacia imekuwa katika mgogoro na serikali ya Tanzania kwa takriban miezi sita sasa tangu serikali izuie usafirishwaji wa makinikia ya kampuni hiyo kwenda nje ya nchi.