Ubelgiji imekuwa taifa la kwanza kutoka Ulaya kujiunga na wenyeji Urusi katika kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi dhidi ya Ugiriki wa 2-1 kupitia mabao kutoka kwa Jan Vertonghen na Romelu Lukaku.

Magoli yote matatu yalifungwa katika dakika tano kipindi cha pili, Vertonghen akitangulia kwa kuiweka Ubelgiji kifua mbele.

José Carlos Gonçalves Rodrigues, almaarufu kama Zeca alipatia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 73 lakini dakika ya 74 Lukaku akafungia Ubelgiji bao la ushindi kwa kichwa.

Ubeligiji wanaongoza katika kundi H na alama 8 wakiwa bado na michezo miwili ya kucheza.

Ubelgiji wamejiunga na Brazil, Iran na Japan katika kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia , huku Urusi wakijipatia nafasi ya moja kwa moja kwa kuwa ni wenyeji wa michuano hiyo.

Bosnia-Herzegovina imeipita Ugiriki na kujipatia nafasi katika michezo ya kufuzu kwa muondoano.

Hii ni baada ya Edin Dzeko kufunga magoli mawili yaliowapatia ushindi wa magoli 4-0 huko Gibraltar na kujinyakulia nafasi ya pili katika kundi hilo nyuma ya Ubelgiji.

Magoli mengine yalifungwa na Kenan Kodro na Senad Lulic upande wa vijana hao wanaonolewa na Mehmed Bazdarevic ambao wako na alama 14, alama moja zaidi ya Ugiriki.

Uswizi ilisalia na alama tatu mbele ya mabingwa wa Ulaya, Ureno baada ya wote kupata ushindi siku ya Jumapili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *