Mwanamuziki wa bongo Fleva, Dogo Janja ambaye sasa hivi anafanya vizuri kwa kazi yake mpya ya ‘Ngarenaro’, ameamua kurudi shule baada ya muda mrefu wa kukacha masomo.
Madee ambaye ndiye msimamizi wa Dogo Janja amesema kwamba mpango huo utaanza mwakani ambapo msanii huyo atarudia mtihani wa kidato cha nne, ili aweze kusonga mbele kielimu, kwani ni kitu muhimu kwenye maisha.
Madee amesema kuwa “Kikubwa ambacho anataka yeye afanye mtihani wa kidato cha nne apate cheti, unajua elimu itabakia kuwa ni elimu, ukisema aache aendelee na ujanja ujanja wa mjini sio ishu ya kufanya, elimu ukiwa nayo unakuwa umejiwekea hazina mbayo ukitaka kufanya kitu fulani unafanya unaendesha maisha vizuri, hivi vitu vingine tunabahatishaga tu”,.
Madee amesema kwamba kutokana na jambo hilo msanii huyo atakuwa kimya kwa muda wa mwaka mzima ili awe makini na masomo, na atarejea kwenye game baada ya kuhitimisha analokusudia.
Dogo Janja aliacha shule akiwa kidato cha pili baada ya kufeli mtihani wa ukuingia kidato cha 3, lakini amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki kwa kazi zake ambazo amekuwa akitoa tangu arudi kwenye game.