Mapigano hayo yamejiri wiki moja baada ya rais wa Sudan Kusini kumuapisha makamu wa kwanza mpya Taban Gai.
Wasemaji wa pande mbili wamekua wakilaumiana kwa mashambulio.
Msemaji wa SPLA, Lul Ruai Koang amesema kwamba mapigano yalishika kasi mwishoni mwa wiki, maili tisini kaskazini mashariki mwa mji mkuu Juba, baada ya mashambulizi ya makombora kutoka kwa majeshi ya upinzani kutoka maeneo matatu tofauti.
Vikosi vya upinzani kutoka SPLA vilivyojitenga na serikali vinalaumu serikali kwa kukusanya majeshi na kutuma helikopta za kivita kumsaka aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar, aliyetoroka juba vita vilipoanza.