Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wauguzi na madaktari kuwa wavumilivu wanapotoa huduma kwa wagonjwa licha ya changamoto ambazo wanazo zipata wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Makonda amesema hayo jana alipokwenda kutembelea hospitali mpya ya mama na mtoto iliyopo Chanika wilayani ilala jijini Dar es Salaam.

Makonda amewataka madaktari na wauguzi hao kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kuwahudumia wote bila ya kujali rangi,sura,wala kabila na hata uwezo wa kipato chake.

Makonda amesema kuwa β€œWapo wakina mama ambao watakao kuja wakiwa na hasira na kukujibu majibu yasiyo mazuri , wengine utakuta wanakusonya tu bila sababu yeyote ,mwengine anweza hata kukutemea mate, basi chukulia ni moja ya sehemu yako ya kazi wala usijibizane nae”.

Hospitali hiyo imengwa na wadau wa maendeleo kutoka Korea kusini, ambapo hospitali hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na hivi karibuni itaanza kutoa huduma kwa mama na mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *