Mawakili wa upinzani nchini Kenya katika mawasilisho yao kwenye Mahakama ya Juu mawakili James Orengo na Otiende Amolo wamesema kwamba Chebukati alimtangaza Rais Kenyatta mshindi siku nne kabla ya kupokea matokeo kutoka maeneo yote kinyume cha sheria za uchaguzi.

Ukweli zaidi utaanikwa baada ya mitambo ya kupokea na kupeperusha matokeo kufunguliwa kubaini jinsi kura kutoka vituo visivyo rasmi zaidi ya 10,000 vilivyotumwa katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha matokeo ya kura za urais (NTC) cha Bomas jijini Nairobi.

Wakati huo huo mawakili hao wamefichua, kufikia sasa Chebukati hakutangaza idadi ya kura zilizoharibika za kila mmoja wa wawania kiti cha urais inavyotakiwa kisheria.

Amesema kuwa Agosti 11 kura zilizokataliwa na kuharibika ni 477,000 kisha akasema mnamo Agosti 18 kura zilizoharibika ni 403,003 na mwishowe akasema kura zilizoharika ni 81,685.

Aliongeza kufikia Agosti 11 Chebukati alikuwa amepokea Fomu 34A 29,000 kutoka kwa maafisa wa IEBC ikiwa ni nusu ya Fomu zaidi ya 40,883.

Majaji hao walifahamishwa  kuwa kura zaidi ya 7 milioni kutoka vituo visivyo rasmi vya kupigia kura zilitumwa katika kituo cha kitaifa cha kujumulisha kura (NTC) kutoka vituo 10,480.

Pia mahakama ilifahamishwa kuwa kura za Odinga ziliibwa na maafisa wa IEBC na kujumulishwa katika kura za Rais Kenyatta na maafisa wa IEBC.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *