Kampuni ya Acacia kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.
Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita.
Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na kuanza kufanya kazi.
Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.
Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.