Kesi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini  (TFF), Jamal Malinzi imeendelea leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Upande wa Jamal Malinzi na wenzake,  umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa maelekezo mahsusi kwa upande serikali kuharakisha upelelezi dhidi ya washitakiwa, kinyume na hapo mahakama iwasikilize na iwaachie huru.

Wakili wa utetezi, Domician Rwegoshora,  amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri,  kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani wanateseka.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis Peter,  akasema kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu kesi itaanza kusikilizwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 9, mwaka huku akiutaka upande wa serikali kuharakisha na ikiwezekana katika tarehe hiyo watoe taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *