Shirikisho la soka nchini TFF limeomba radhi kwa mashabiki wa soka kufuatia makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa jana.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini.

Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.

TFF wamesema kuwa hawajapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *