Jeshi la Polisi limemaliza  upekuzi waliokuwa wanafanya nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu  Lissu  wanaelekea  Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam.

Taarifa ya msemaji wa Chadema Tumaini Makene amesema Lissu anapelekwa polisi  kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria kuendelea  ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo kisheria iko wazi.

Amesema upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo  ya kumkashifu  rais na  Uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.

Tundu Lissu alikamatwa jana akiwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kosa la uchochezi kuhusu ndege za Bomberdier.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *