Mkali wa Rhymes, Afande Sele amefunguka kwa kusema kuwa vijana wa kiume kujihusisha katika mapenzi na wakubwa zao ili kusaidiwa kiuchumi ni moja ya sabubu zinazopelekea upungufu wa nguvu za kiume.
Afande Sele ametoa kauli hiyo baada ya kukithiri kwa vitendo vya vijana wenye umri mdogo kutoka kimapenzi na wamama watu wazima kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi.
Afande Sele ameeleza kuwa kitendo hicho kinamnyima uhuru binafsi muhusika kwa sababu unapokaa na mtu ambaye kila kitu unamtengemea unakosa uhuru wa maisha.
Afande Sele amesema kuwa vitendo hivyo vinasababisha wavulana kupoteza uwezo wa kufikiria kutokana na muda mwingi kuwaza kumfuraisha mpenzi wake kuliko kufikiria maisha yake.
Ameendelea kusema kuwa muda mwingine hata mapenzi unakuta hujisikii kwa sababu mapenzi nayo ni ratiba lakini kwa sababu unaishi na mtu anakulea utafanya tu.
Pia Afande Sele amesema kuwa ndio maana leo hii suala la nguvu za kiume limekuwa ni agenda kubwa kwa sababu wanafanya vitu na watu siyo machaguo yao.