Mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye ligi kuu Ufaransa baada ya kufunga goli mbili kwenye ushindi wa 6-2 dhidi ya Toulouse jana.

Neymar mwenye umri wa miaka 25 aliifungia PSG bao la kusawazisha, baada ya Max Gradel kuifungia Toulouse bao la kuongoza dakika ya 18.

Adrien Rabiot aliongeza bao la pili kabla ya Edinson Cavani hajafunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati.

Bao la nne la PSG lilikwamishwa wavuni na Marco Verratti dakika ya 69, lakini Toulouse wakapata goli la pili kupitia kwa Christopher Jullien na kwa upande wa goli la tano likafungwa na Javier Pastore.

Neymar alimaliza kupigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la sita na kukamilisha ushindi wa tatu mfululizo kwa PSG katika ligi ya nchini Ufaransa.

Ushindi huo unaiwezesha PSG kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini Ufaransa kwa kufikisha point 9, sawa na mabingwa watetezi AS Monaco ambao wanazidiwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *