Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amewasili nyumbani katika mji mkuu Abuja, baada ya likizo ya matibabu ya miezi mitatu mjini London.

Wafuasi waliimba na kucheza densi walijipanga kwenye barabara za mji, ambapo maafisa wa ngazi za juu serikalini walikusanyika kumkaribisha Buhari.

Haijulikani ikiwa Buhari atarejea shughuli zake kamili kama rais kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuugua.

Amefanya safari ya kupata matibabu London mara tatu tangu mwezi Juni mwaka uliopita kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Anatarajiwa kuhutubia taifa siku ya Jumatatu asubuhi huku kukiwa na maandamano ya kumtaka Buhari arudi nyumbani au ajiuzulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *