Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya (CHADEMA) amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Mara.
Mbunge huyo amekamatwa akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo.
Kamanda huyo amesema kuwa wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Tarime.