Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ameahidi kumsomesha kijana mmoja baada ya kuonyesha uwezo wa juu katika somo la hesabu licha ya kusoma katika shule yenye changamoto.

Waziri Nchemba ameshuhudia uwezo wa mwanafunzi huyo akiwa wakati alipoingia shuleni hapo na kuanza kufundisha somo la hesabu ambapo amefurahishwa na jinsi walimu wa shule hiyo walivyojitahidi kuweka juhudi zao katika kuhakikisha wanawasaidia watoto hao kutimiza malengo yao.

Waziri Nchemba akiwa kwenye ziara ndani ya jimbo la Iramba alipita shuleni hapo kusikiliza kero mbalimbali lakini pia kufuatilia hali ya taaluma ndani ya jimbo la Iramba ambapo ameshuhudia miundombinu mibovu inayohatarisha usalama kwa wanafunzi waliopo shuleni hapo na kuahidi kuirekebisha mapema iwezekanavyo.

Akiwa shuleni hapo Mh. Waziri ameahidi kujitolea kujenga nyumba za walimu pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa ambavyo vinahatarisha usalama wa wanafunzi hao.

Waziri Mwigulu ametoa ahadi hiyo baada ya kutembelea shule hiyo na kusema mazingira wanayopitia waalimu pamoja na wanafunzi hao ni magumu sana ingawa walimu wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi hao wanafanya vizuri na kufikia ndoto zao.

Waziri Nchemba ameshuhudia waalimu wanaokadiriwa kuwa tisa wa shule hiyo wakiishi pamoja katika nyumba chache zilizopo shuleni hapo huku vyumba vya madarasa  navyo vikiwa si vyakuridhisha sana.

Waziri Mwigulu ameshuhudia ubovu wa madarasa matatu ya shule hiyo yakiwa mabovu kabisa na yenye nyufa kubwa ambayo ni hatari sana kwa usalama wa wanafunzi huku madarasa hayo yakiwa hayana sakafu kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *