Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moni Centralzone amejibu tuhuma zinazomkabili za kuiba wazo la wimbo wake wa ‘Matango Pori’ kutoka kwenye wimbo wa ‘Matango Nyanya’ wa H Mbizo.
Moni amekana tuhuma hizo na kueleza kuwa kilichofanana kwenye nyimbo hizo ni maneno machache tu na sio wazo zima na uandishi.
Moni amesema hakuna ukweli kuhusu kuiba wazo la wimbo huo kutokana na wimbo huo ametunga mwenyewe.
Mwanamuziki amesema kuwa “Kwanza mimi naona huu ni msaada kwa H Mbizo kwasabubu watu wanapozungumzia wimbo wangu wanazungumzia na wimbo wake,” alisema.
Mwisho amemalizia kusema kuwa “H Mbizo ni kaka yangu lakini hajawahi kunishawishi mimi kufanya muziki mpaka kufikia hatua ya kumuibia wazo la wimbo au hata wimbo mzima,” aliongeza.