Mahakama Kuu imeahirisha kutoa hukumu juu ya pingamizi lililowasilishwa na wabunge wanane wa Viti Maalum wa CUF kupinga Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaapisha wabunge wapya walioteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano anayeunga mkono upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande, kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotoa uamuzi kuhusu suala hilo.
Maharagande aliyasema hayo alipoongea na waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya mahakama hiyo.
Wabunge hao walivualiwa uanachama na mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Lipumba kutokana na kukiuka katiba ya chama hicho.