Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda anatajia kuendesha kongamano katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) Posta kujadili hali za barabara za jiji la Dar es salaam ambapo wananchi watapewa fursa za kueleza hali za barabara kutoka mitaani kwao.

Makonda amesema kuwa kongomano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa barabara wakiwemo Tanroad, wakandarasi pamoja na wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Mapema wiki hii RC Makonda akiwa katika kikao na Bodi ya Barabara, alisema kuwa hataki kuona kwenye mkoa wake barabara zinatengenezwa kwa gharama kubwa halafu zinaharibika kwa muda mfupi na kusababisha Kero kubwa kwa watumiaji wa Barabara.

RC aliwataka wajumbe wa bodi hiyo kuhakikisha wanazuia uharibifu wa barabara unaofanywa magari yanayobeba mizigo mikubwa kupita uwezo wa barabara.

Amesema katika bajeti ya serikali ya mwaka 2017 -2018 imetengwa zaidi ya shilingi Billion 184 kwaajili ya ujenzi wa barabara za mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 5%.

Pia Makonda aliziagiza makampuni zote zitakazofanya kazi ya ukamataji wa vyombo vya moto na kufanya kazi hiyo kinyume na mkataba hali inayoleta kero kwa wananchi kuvunja mikataba yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *