Kesi inayowakili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamo wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imehairishwa tena leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaama.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 30 mwaka huu utokanan na upepelezi kutokamilika dhidi ya tuhuma za viongozi hao.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Victoria Nongwa baada ya Wakili wa upande wa mashitaka kueleza kuwa kwa vile nyaraka za kughushi maandiko zinahitaji utaalam kuzibaini, hivyo kitengo maalum cha kubaini maandishi kinaendelea kufanya uchunguzi ili kukamilisha upelezi huo ambapo aliomba kesi hiyo isogezwe mbele kwa siku 14 ili kukamilisha uchunguzi.
Hakimu Victoria Nongwa aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha haraka upelezi wao ili kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo aliisogeza hadi Agosti 30 ili kuwapa nafasi kukamilisha upelelezi wao huku watuhumiwa wakirudishwa gerezani.
Viongozi wa hao wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.