Wafuasi wa upinzani wamekusanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kupinga uwezekano kuwa uchaguzi wa rais huenda ukaahirishwa nchini humo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanywa Novemba mwaka huu, lakini tume ya uchaguzi, imesema inaweza kuchukua miezi 16, kurekibisha orodha za wapigaji kura.

Upinzani unaona kuna jaribio la kuahirisha uchaguzi ili kumruhusu rais Joseph Kabila abakie madarakani.

Kufuatana na katiba ya nchi hiyo Rais Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu, baada ya kutumika kwa mihula miwili.

Hata hivyo mahakama ya kikatiba nchini humo imeamua abakie madarakani, hadi uchaguzi utapokafanywa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *