Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza CV za watendaji kata za Dar es Salaam zipitiwe upya kwani haridhishwi na utendaji wa kazi zao.
Makonda ametoka kauli jana katika eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku 4 kutatuliwa kero za eneo hilo.
Mkuu wa mkoa huyo alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza mkuu wa Wilaya ya Kindondoni Ally Happi kukagua Cv za watendaji wake wa kata.
Amedai watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na hatimaye wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogo madogo yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko.
Juzi Wakati Rais Magufuli anarejea Jijini Dsm kutoka Mkoani Tanga alikokuwa kwenye ziara yake ya siku tano, alisimamishwa na wananchi wa Bunju B katika wilaya ya Kinondoni na kumueleza kero zao na baada ya hapo Rais Magufuli alitoa agizo la ndani ya siku nne Mkuu wa mkoa Makonda awe amefika na kutoa majibu ya kero hizo.