Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amesema kuwa hana mpango wa kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2020.
Kauli imekuja baada ya kuenea taarifa kuwa Meya huyo wa Ubungo anajiandaa kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Amesema kuwa anaimani na utendaji kazi wa mbunge wa jimbo hilo, Saed Kubenea hivyo haoni sababu ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha kugombea nafsi hiyo ya ubunge.
Ameongeza kwa kusema kuwa atawania nafasi ya ubunge endapo litaanzishwa jimbo jipya kwani hadi sasa anaridhishwa na utendaji kazi wa mbunge wa jimbo hilo, huku akisema suala la maendeleo linahitaji mshkamano.
Majimbo yanayoongozwa na wapinzani ni pamoja na Kibamba (John Mnyika), Kawe (Halima Mdee), Ubungo (Saed Kubenea), Kinondoni (Maulid Mtulia), Abdallah Mtolea (Temeke) na Ukonga ni Mwita Waitara.