Shirika la ndege la Algeria limewakuza kazi marubani wake wawili baada ya kumruhusu mtoto mwenye umri wa miaka mitano kuendesha ndege ya abiria.
Marubani hao wawili wamekuzwa kazi kutokana na kosa hilo ambapo wangeweza kuhatarisha uhai wa abiria.
Mtandao wa Africa News unasema kuwa zoezi hilo liifadhiliwa na kurekodiwa na runinga ya El Bilad TV waliomuonyesha mtoto huyo akiwa amavaa sare za rubani akibofya vitufe katika chumba cha rubani.
Haijulikani ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Air Algerie kutoka mji wa Algiers hadi mji wa Setif.
Mtandao huo umesema kuwa rubani hao walifukuzwa kazi Julai 29 mwaka huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa sababu kitendo hicho kilikiuka sheria za usafiri wa ndege.